Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA-
Leo hii (Jumamosi), tarehe: 12/7/2025 | sawa na tarehe 16 / Muharram / 1447Hijria, kimefanyika kikao cha Kielimu na Utafiti kuhusu "Kumjua Mwenyezi Mungu (swt) Kujifunza Kuhusu", washiriki wakiwa ni Wanafunzi wote wa Madrasa ya Hazrat Zainab (sa) iliyopo Kigamboni Jijini Dar-es-salaam. Mtafiti katika Kikao ni: Samahat Sheikh Ghawth Nyambwa. Na mratibu wa Kikao hiki cha Kielimu ni: Kitengo cha Hawza ya Wasichana ya Hazrat Zainab (sa).
Katika kikao hiki cha kielimu kilichoandaliwa na Kitengo cha Wasichana, Samahat Sheikh Ghawth aliongoza mjadala wa kina kuhusu njia na dalili za dhahiri katika kumjua Mwenyezi Mungu(swt).
Akinukuu Aya ya 108 ya Surah Yusuf, Sheikh Ghawth alisisitiza umuhimu wa kutumia akili, mazingatio na dalili za ulimwengu wa nje (Ulimwengu wa Dhahiri) katika kumuelewa Muumba.
Baada ya uwasilishaji wake wa mada, aliendelea kujibu maswali ya Wanafunzi kuhusu masuala mbalimbali ya Tauhid, na kwa namna hiyo akakamilisha kikao hicho kwa mafanikio.
Kikao kilikuwa na manufaa makubwa kwa washiriki, kwani kilitoa mwanga zaidi juu ya misingi ya imani na mbinu za kielimu katika kumjua Mwenyezi Mungu(swt).
Your Comment